BIASHARA YA MTUMBA. (WATOTO)
BIASHARA YA NGUO ZA MITUMBA ZA WATOTO (Mwongozo) Hii biashara ina faida sana ila kama ilivyo kwa biashara zote uchaguzi wa Eneo ni muhimu,lakini pia hata bila kuwa na eneo ili mradi ukipata mawasiliano na watu unaolenga kuwafanya wateja wako na kuweza kuwaletea nguo za watoto quality kulingana na mahitaji yao basi waweza ukamudu soko la mitumba ya watoto. π️Nguo za watoto miaka 0-4, zitakutoa hasa wa kiume, bukta za jeans, vigauni ya wakike pia vinalipa, kumbuka watoto huvalishwa nguo zaidi ya nne kwa siku, hujikojolea kujichafua kwahiyo wanahitaji nguo nyingi kuliko rika lingine. π️NGUO za watoto utakayo muuzia MWANAUME ni bei ya juu kuliko MWANAMKE sababu ni kwa kuwa wanaume wengi hawajui bei za nguo kama akina mama. π©Pia NGUO ZA WANAWAKE HASA WADADA ZINALIPA kumbuka wanaume hawana tabia za kununua nguo kama wanawake. π️(Bale)Robota moja la nguo za watoto lina nguo 300 au 400 na kuendelea linauzwa GRADE Three 220,000/= G...