RICHEST PERSON IN BABEL (SWAHILI VERSION)
SIMULIZI:
đź“–:
Mtu Tajiri wa Babeli
Lugha: Kiswahili
Kurasa: 147
Fomat: PDF
MAUDHUI:
Elimu, Kanuni na Miongozo thabiti ya mafanikio ya kifedha na Maisha kwa kutumia simulizi za kweli za kusisimua zilizothibiti katika mji tajiri zaidi kutokea duniani, mji wa Babeli (Babylon),mji ambao ulikuwa na idadi kubwa ya matajiri kuliko mji wowote ule zaidi ya miaka 5000 iliyopita.
Miongozo na kanuni ambazo mpaka leo hii zinatumiwa na matajiri pamoja na taasisi za kifedha kama vile mabenki, Bima na Taasisi za ukopeshaji fedha katika kujipatia, kujiongezea na kuhifadhi mali na fedha.
Ni kitabu kinachotoa miongozo na kanuni za uwekaji akiba, uwekezaji wa kibiashara,njia za kujikwamua na mikopo, njia za kudhibiti utapeli, njia za kupambana na changamoto za utafutaji fedha, njia za kujikwamua na umaskini na kuelekea kwenye utajiri, Taaluma na ulaghai wa kamari (betting) na mengine mengi.
1 *
MTU TAJIRI ZAIDI NDANI YA BABELI
Katika mji wa kale wa Babeli aliishi bwana mmoja tajiri sana aliyejulikana kwa jina la Arkad. Pande zote za mji alikuwa ni maarufu kutokana na utajiri wake mkubwa pamoja na busara zake. Umaarufu wake ulizidi kuongezeka kutokana na ukarimu wake kwa watu, pia alikuwa ni mwepesi sana katika kutoa misaada kwa watu mbalimbali. Pamoja na yote,pia alikuwa ni mtu mwenye kuijali na kuipatia familia yake kila ilichohitaji. Alikuwa ni mtu asiye na mawazo katika matumizi yake kwani alikuwa akitumia apendavyo, lakini pamoja na matumizi yote hayo kila mwaka utajiri wake ulizidi kuongezeka maradufu.
Ghafla wakaingia marafiki zake wa siku nyingi sana, urafiki wa tokea enzi za ujana wao. Akawakaribisha kisha moja wao akaanza kwa kusema, “ Arkad, wewe ni mtu uliyebahatika na kufanikiwa kimaisha kuliko sisi. Umejaaliwa utajiri mkubwa kupita mtu yeyote ndani ya babeli hii, wakati huhohuo sisi rafiki zako tunahangaika angalau kupata chochote cha kutufanya tuweze kuiona siku ya kesho. Unavaa majoho ya kupendeza huku ukifurahia kula vyakula vitamu na adimu, wakati sisi mioyo yetu imejawa na dhiki na kujawa na hofu hata ya kuweza kuvisha familia zetu mavazi yenye kueleweka pamoja na kuwapatia chakula cha kutosha."
“Kuna kipindi hali zetu zilikuwa zinafanana. Wote tulisoma kwa mwalimu mmoja na kucheza pamoja. Na hakuna mchezo wala somo moja ambalo ulitushinda, hata siku zilizofuata hujawahi kuwa mtu mwenye kuheshimika zaidi yetu katika mji huu. Pia hukuwahi hata kuwa mchapakazi hodari zaidi yetu. Sasa ni ipi bahati ambayo imekufanya leo hii uishi kwa kufurahia maisha utakavyo tofauti na sisi? Na kututenga sisi ambao pia tunastahili kuwa kama wewe?”
Arkad aliwakatisha na kisha kuwaambia;
"Ikiwa tokea kipindi cha ujana wetu mpaka leo hii bado hamjafanikiwa kupata utajiri ni kwa sababu inawezekana hamkujifunza njia na kanuni zinazoongoza kujipatia mali, ama hamkuzitilia maanani kanuni hizo na kuacha kuzifanyia kazi.
Bahati ni Mungu mkatili sana ambaye hawezi kutoa msaada kwa mtu asiye mjuzi, na pia huwaangusha wale ambao hapo mwanzo walijishughulisha katika kutafuta mali lakini walizitumia wapendavyo, watu ambao walifanya manunuzi hovyo kwa kila walichokiona na kwa kila kipato walichokipata,watu ambao walikuwa na tamaa sana hata kwa vitu ambavyo hawakuwa na uwezo navyo. Pia kuna wale ambao ni wabahili na kutaka kujilimbikizia mali wakiogopa kuzitumia kwa kujua kuwa hawana uwezo wa kuzipata tena.
Wengine wanakwenda mbali zaidi na kuogopa kutumia mali zao kwa kuogopa kujulikana kwa kuhofia kuibiwa hizo mali, watu hao wanaishi maisha ya usiri na kuwa kama mafukara.
Pia kuna wale ambao hawakutumia jasho lao katika kuzipata hizo mali, ama kwa kuiba ama kudhurumu huku wakiendelea kufurahia maisha. Ila kuna wachache siwafahamu bali kwa kusikia tu mitaani kuwa wamepata utajiri kwa kurithi ama bila kujulikana walikoutoa."
Rafiki zake walikiri kuwa kuna watu wametajirika kwa kurithi, hivyo maneno yake ni ya kweli kabisa. Kisha wakamuomba awaelezee ni jinsi gani aliweza kuwa tajiri.
Comments
Post a Comment