CAR WASH BUSINESS ( BIASHARA YA KUOSHA MAGARI)

BIASHARA ya KUOSHA MAGARI/CAR WASH (Mwongozo) 
 đź“–Tumekuwa tukiosha magari sehemu mbali mbali bila kupiga hesabu tumelipa kiasi gani na kukadiria iwapo mtoa huduma ameosha magari kumi kwa siku atakuwa amepata kiasi gani.

 đź“ŚChukua kwa mfano kuosha gari ni shilingi 5,000 -7,000, hivyo ukiosha magari kumi kwa siku unaweza ukapata shilingi 50,000-70,000 kwa siku kabla ya kuondoa gharama za kuosha magari. 

 đź“Ť Biashara hii inahitaji usimamizi wa karibu zaidi. Ukiweza kuisimamia vizuri ni biashara yenye faida kubwa hasa ukiweza kuiweka sehemu ambayo watu wanapumzika kwa ajili ya kula au kunywa vinywaji. 

 đź—ť️Biashara ya uoshaji wa magari maarufu kama “car wash” ni biashara ambayo mahitaji yake hutegemea unataka uanzishe biashara ya ukubwa gani. Kwa mfano kuna,
 ✅ Carwash ndogondogo za hali ya chini kabisa, 
✅ Car wash za kati na 
✅ Car wash kubwa za hali ya juu(full car engine and body washing) 

 đź“ŚTukiacha Car wash za hali ya chini kabisa ambazo mtaji wake hauhitaji zaidi ya madumu yako mawili, ndoo, kitambaa na eneo lenye mto au kijito cha maji, 

car wash yeyote ile ya kati au kubwa itahitaji vitu(vifaa) muhimu vifuatavyo;
 1. Pressure washer(Compressors) 
2. Vacuum cleaner 
3. Tanki la maji
 4. Brashi, ndoo, mataulo na vyombo vingine vidogovidogo
 5. Madawa kwa ajili ya kuoshea magari kama shampoo na sabuni 
 đź“–đź—ť️Vilevile vifaa vilivyotajwa hapo juu vipo vya hadhi ya juu sana kutoka nchi za Ulaya na Marekani kama vile, USA, Ujerumani, Ufaransa, na Uingereza(UK). Lakini pia kuna vifaa vya bei chee vinavyofanya kazi kama hiyohiyo vya Mchina. 

 đź—ť️Mfano Pressure washer kutoka Ulaya kama vile KARCHER, BOSCH, SIMPSON nk. huweza kuanzia Tsh. 500,000/= hadi tsh. 2,000,000/= wakati vile vya mchina kutoka nchini China vinavyofanya kazi kama hiyohiyo huanzia tsh. 150,000/= mpaka 200,000/= na kuendelea kutegemeana na aina na ukubwa wake katika vipimo vya Kilowatt au Horsepower. 
Kuna vifaa pia vinavyotumia umeme na vinavyotumia mafuta(dizeli) Hali kadhalika vifaa vinginevyo kama Vacuum cleaner, kuna za kuanzia shilingi za kitanzania 30,000/= mpaka laki 3(300,000/=) na kuendelea kulingana na aina, nchi itokako na ukubwa kama nilivyotangulia kusema. Kutokana na maelezo hayo Uchaguzi utabaki ni kwako uanze na aina ipi ya 'CAR WASH STATION'.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

RICHEST PERSON IN BABEL (SWAHILI VERSION)