BIASHARA YA MTUMBA. (WATOTO)

BIASHARA YA NGUO ZA MITUMBA ZA WATOTO (Mwongozo) 

 Hii biashara ina faida sana ila kama ilivyo kwa biashara zote uchaguzi wa Eneo ni muhimu,lakini pia hata bila kuwa na eneo ili mradi ukipata mawasiliano na watu unaolenga kuwafanya wateja wako na kuweza kuwaletea nguo za watoto quality kulingana na mahitaji yao basi waweza ukamudu soko la mitumba ya watoto. 

 🗝️Nguo za watoto miaka 0-4, zitakutoa hasa wa kiume, bukta za jeans, vigauni ya wakike pia vinalipa, kumbuka watoto huvalishwa nguo zaidi ya nne kwa siku, hujikojolea kujichafua kwahiyo wanahitaji nguo nyingi kuliko rika lingine. 

 🗝️NGUO za watoto utakayo muuzia MWANAUME ni bei ya juu kuliko MWANAMKE sababu ni kwa kuwa wanaume wengi hawajui bei za nguo kama akina mama. 

 🚩Pia NGUO ZA WANAWAKE HASA WADADA ZINALIPA kumbuka wanaume hawana tabia za kununua nguo kama wanawake. 

 🗝️(Bale)Robota moja la nguo za watoto lina nguo 300 au 400 na kuendelea linauzwa GRADE Three 220,000/= GRADE TWO 350,000/= GRADE ONE 600,000/= nyingne ni 800,000/= 

 📌Bei ni za DAR ES SALAM na maeneo yanauzwa Bales za mitumba:- 

 📍Ukifika Mnazi Mmoja dar, kama unatoka k.koo nyooka moja kwa moja kama unaenda mnara wa saa au stesheni, unapovuka tu makutano ya pili ya mataa, ya mnazi mmoja kuna maduka wanauza sana kanga na vitenge, kuanzia hapo, maduka ya mitumba nikibao, nenda mtaa wa pili kama sikosei unaitwa sofia, maduka kibao hapo mitumba tupu, yani zunguka eneo ilo utapata mitumba kibao. 

 📍Pili ukiwa Congo, K.koo kituoni mkono wa kulia ukiwa unaelekea mnazi lipo duka moja hapo kwa mhind linapakana na duka la Samsung. 

 📍Tatu Magomeni, ni eneo jipya hili, ofis za TTCL ukifika hapo upande wa pili utaona mitumba hadi ya viatu wholesale bales.Pale magomeni ni makutano ya mataa pale ukiuliza ofis za TTCL utaoneshwa. 

 📍 Pia kuna Soko la Mnada wa mitumba pale KARUME fanya kuwahi asubuhi sana saa 10 alfajiri ukachague. 

 🚫 TAHADHARI: Ufunguapo Bale la mitumba ni sawa na nazi hujui kama ni nzima au mbovu ndani, UNAWEZA NUNUA UKAPATA NGUO NZURI MPAKA RAHA siku nyingne ukanunua zote mbovu haziuziki hata moja ndo BIASHARA ILIVYO ​

 📍Balo zipo sehemu nyingi. 
CHANGAMOTO ni iyo uchakachuzi wa bales. Mara nyingi bale ikiwa na koa, imefungwa na yale mabati inakuwa haijafunguliwa, ila ikiwa na plastic mara nyingi izo ndizo zimefungwa upya, ila si lazima iwe ivo. 
 CHANGAMOTO ni kupata bales nzuri, kama unaweza mtafute (muuzaji mitumba mzoefu) ambaye wanampa vitu bora katika maduka hayo ya jumla, akuchukulie. Au washikishe wale jamaa tingo wa dukani kitu kidogo, wambie nipe kitu cha maana jifanye ni mzoefu ila umebadili duka tu na kwenda hapo kwao. Ukijifanya mzoefu usizubae, kwa mfano ukiuliza mixer ya nguo za kike, akikuuliza kg ngapi unakuwa shapu kuonesha unajua, sio wanauliza Kg hujui kuwa bales zina kilogram. Au unaulizwa material unayotaka hujui, either cotton, nylon n.k 

 *Note:* Iko hivi Bales za mitumba huuzwa kwa kilogaram,mfn Bale la kg 100 huuzwa hadi mil 1 kulingana na Grades pia. Unaweza ukatembelea maeneo ya masoko ya Bales za Mitumba niliyoorodhesha hapo juu ukathibitishe na kujifunza zaidi...

Comments

Popular posts from this blog

RICHEST PERSON IN BABEL (SWAHILI VERSION)

CAR WASH BUSINESS ( BIASHARA YA KUOSHA MAGARI)