CAR WASH BUSINESS ( BIASHARA YA KUOSHA MAGARI)
BIASHARA ya KUOSHA MAGARI/CAR WASH (Mwongozo) ๐Tumekuwa tukiosha magari sehemu mbali mbali bila kupiga hesabu tumelipa kiasi gani na kukadiria iwapo mtoa huduma ameosha magari kumi kwa siku atakuwa amepata kiasi gani. ๐Chukua kwa mfano kuosha gari ni shilingi 5,000 -7,000, hivyo ukiosha magari kumi kwa siku unaweza ukapata shilingi 50,000-70,000 kwa siku kabla ya kuondoa gharama za kuosha magari. ๐ Biashara hii inahitaji usimamizi wa karibu zaidi. Ukiweza kuisimamia vizuri ni biashara yenye faida kubwa hasa ukiweza kuiweka sehemu ambayo watu wanapumzika kwa ajili ya kula au kunywa vinywaji. ๐️Biashara ya uoshaji wa magari maarufu kama “car wash” ni biashara ambayo mahitaji yake hutegemea unataka uanzishe biashara ya ukubwa gani. Kwa mfano kuna, ✅ Carwash ndogondogo za hali ya chini kabisa, ✅ Car wash za kati na ✅ Car wash kubwa za hali ya juu(full car engine and body washing) ๐Tukiacha Car wash za hal...